Athletic Bilbao yatwaa Super Cup

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Athletic Bilbao mabingwa Super Cup

Klabu ya soka ya Athletic Bilbao imetwaa ubigwa wa kombe la Super Cup nchini Hispania baada ya kwenda sare ya kufunga bao 1-1 na Barcelona.

Bilbao wametwaa ubingwa huo baada ya miaka 31 katika mchezo ulichezwa katika dimba la Nou Camp.Katika mchezo wa fainali ya kwanza uliochezwa kwenye dimba la San Mames Bilbao walipata ushindi wa mabao 4-0.

Mshambuliaji Lionel Messi ndio alianza kuiandikia timu yake bao dakika 44 kabla ya Aritz Aduriz kuisawazishia timu yake katika dakika ya 81 ya mchezo na na kuihakikishia ubingwa huo kwa jumla ya mabao 5-1.

Beki wa Barca Gerard Pique na Kike Sola wa Bilbao walipewa kadi nyekundu katika mchezo huo.