West Brom yakataa kumtoa Berahino

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Saido Berahino alikuwa mshambuliaji watatu kwa ufungajji kwa wachezaji raia wa Uingereza

Klabu ya soka ya West Bromwich albion, imekataa dau la pauni milioni 15 toka kwa timu ya Tottenham, inayohitaji saini ya mshambuliaji Saido Berahino.

Berahino mwenye miaka 22, amekua katika mawindo ya kocha wa Spurs Mauricio Pochettino, ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

Mwenyekiti wa West Brom Jeremy Peace, amemwambia mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy, hawako tayari kuuza mshambuliaji huyo kwa dau hilo la pauni milioni 15.

Klabu hiyo ya West Brom, inasema thamani ya mshambuliaji wao ni pauni milioni 25.

Berahino alikua mshambuliaji watatu kwa ufungaji kwa wachezaji raia wa Uingereza akiwa nyuma ya Harry Kane na Charlie Austin.