Meneja wa Bournemouth alia na mwamuzi

Image caption Eddie Howe

Meneja wa klabu ya Bournemouth ya nchini Uingereza,Eddie Howe amesema maamuzi yaliyofanywa kinyume na matarajio ya wengi katika mchezo waliopoteza dhidi ya Liverpool hayasameheki.

Christian Benteke alifunga goli pekee baada ya kupata kross safi kutoka kwa Jordan Henderson ambayo kabla ya hapo Philippe Coutinho alikwisha otea licha ya kutougusa mpira.

Mapema mchezaji wa Bournemouth Tommy Elphick alikaribia kufunga lakini alinyimwa kwa kucheza vibaya.''Huwezi kupingana na maamuzi na mambo hayo yalitunyima alama muhimu'' alisema meneja wa Bournemouth mwenye miaka 37 Eddie Howe.

Howe alisema kuwa atajaribu kutizama nini kitafuatia kwa mwamuzi wa mchezo huo Craig Pawson pamoja na waaamuzi wasaidizi. Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Anfield, Liverpool waliondoka na ushindi mwembamba wa goli 1 kwa bila lililofungwa na mshambuliaji mpya wa timu hiyo Christian Benteke.