Europa:Borrusia, Sparta zaanza vyema

Image caption Borrusia yatoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 4 dhidi ya 3 ya Odds BK

Timu za Borrusia Dortimund na Sparta Prague, zimeanza vizuri michezo ya kwanza ya mchujo kuwania tiketi ya kushiriki Europa ligi.

Borussia wakicheza ugenini nchini Norway wameibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya klabu ya Odds Bk, mabao ya wajerumani hao yalifungwa na Pierre Eric Aubameyang dakika ya 34, Shinji Kagawa na Mkhitaryan 84′.

Sparta Prague wakiwa katika dimba lao la nyumbani wakapata ushindi wa mabao 3-1dhidi ya FC Thun.

Southampton, wakiwa nyumbani St Marys, wakakubali kwenda sare ya bao 1-1 dhidi FC Midtjylland.

Matokeo mengine ya michezo hiyo Astra Giurgiu 3 – 2 AZ Alkmaar

Dinamo Minsk 2 – 0 FC Red Bull Salzburg

FK Qabala 0 – 0 Panathinaikos

Ajax 1 – 0 FK Jablonec

Molde 2 – 0 Standard Liege