Tanzania wenyeji Fainali Afrika - 2019

Image caption Jamal Malinzi

Tanzania inatarajia kuwa wenyeji wa fainali za Afrika za soka kwa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019.

Akizungumza na BBC leo jijini Dar es salaam Rais wa shirikisho la soka la Tanzania (Tff) Jamal Emmily Malinzi amethibitisha kuwa Tanzania watakuwa wenyeji wa fainali hizo .

Amesema Tff kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania walituma maombi katika shirikisho la soka la Afrika (CAF) kuomba kuwa wenyeji wa fainali hizo na hatimaye Caf imeridhia Tanzania kuwa wenyeji mashindano hayo.

Na shirikisho la soka Tanzania (Tff) likiwa katika mikakati ya maandalizi ya fainali hizo, Rais huyo amewataka wadau mbalimbali wa soka nchini Tanzania yakiwemo mashirika ya watu binafsi , sekta binafs i kujitokeza na kutoa michango ya fedha na vifaa kwa lengo la kufanikisha fainali hizo na hatimaye kuweza kujitangaza kisoka kupitia fainali za afrika kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 17.