Taifa stars kupiga kambi Uturuki

Image caption Timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itaondoka nchini siku ya jumapili kuelekea Istambul nchini Uturuki.

Stars wataweka kambi kwa muda wa siku nane kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria utakaocheza Septemba 5 mwaka nchi Tanzania..

Awali Taifa Stars ilikua ipitie Muscat nchini Oman kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya nchi hiyo, lakini kutokana na shirkikisho la Soka la Oman kushindwa kukidhi mahitaji ya Kanuni za FIFA za uandaaji wa mechi ya kimataifa ya kirafiki sasa mchezo huo hautakuwepo tena.

Stars itaondoka na shirika la ndege la Uturuki na kuwasili Istambul siku ya jumatatu majira ya saa 5 kamili asubuhi, kisha kuelekea Kocael katika hoteli ya Green Park Kartepe ambapo ndio itakua kambi yake ya wiki moja.