Cuba yailaza Kenya katika kombe la dunia

Image caption Kenya sasa imeratibiwa kuchuana dhidi ya jamhuri ya Dominica siku ya jumapili katika mechi yao ya pili.

Wawakilishi wa Afrika katika kombe la dunia la mchezo wa voliboli Kenya wameambulia kichapo katika mechi yao ya ufunguzi seti 3-1 mikononi mwa Cuba.

Malkia strikera ya Kenya iliandikisha matokeo ya alama (27-25, 25-23, 13-25, 25-22) katika mechi ngumu iliyochezewa katika ukumbi wa ndani wa uwanja wa kitaifa wa Yoyogi ulioko Japan.

Mchezaji bora wa katika mechi hiyo alikuwa kutoka Kenya Mercy Moim aliyefunga alama 26.

Mshambuliaji wa Cuba Gracia Gonzalez aliiasidia timu yake kushinda alipoifungia alama 25.

Image caption Cuba yailaza Kenya katika kombe la dunia

Kenya ilianza mechi hiyo vizuri ikiongoza kwa alama 12-8 katika seti ya kwanza kabla ya Cuba kujifurukut na kusawazisha alama 19 kwa 19 kabla yao kuibuka kidedea kwa alama

27-25.

Katika seti ya pili David Lung’aho alifanya mabadiliko lakini wapi , Cuba waliendeleza msururu wa matokeo mema na walikuwa mbele kufikia hatua ya mapumziko wakiwa na alama 16-14.

Cuba iliibuka mshindi wa seti hiyo kwa alama 25-23.

Kenya ambao ndio mabingwa wa dunia wa nishani ya dhahabu ya Grand Prix walijifunga kibwebwe katika seti ya tatu na wakaibuka washindi wa seti ya tatu alama

25-12 .

Hata hivyo waliendelea kufaidi makosa ya timu ya Kenya na wakaibuka washindi wa seti ya nne.

Kenya sasa imeratibiwa kuchuana dhidi yaDominica siku ya jumapili katika mechi yao ya pili.