Van Gaal; Man U haihitaji mshambuliaji

Haki miliki ya picha PA
Image caption Van Gaal; Man U haihitaji mshambuliaji

Meneja wa Manchester United amesema kwamba hana haja ya kuimarisha washambuliaji wake baada ya timu yake kutoka sare 1-1 na Newcastle

Manchester United wamefunga mabao mawili tu katika mechi tatu ambazo wamecheza katika ligi kuu ya Uingereza kufikia sasa.

Mshambuliaji Wayne Rooney hajafanikiwa kuona wavu kutoka tarehe 4 mwezi Aprili

United ilikuwa na matumaini ya kumsajili Pedro, kabla ya mshambualiaji huyo kundoka Barcelona na kujiunga na wapinzani wao sugu Chelsea.

Alipoulizwa kama alihitaji kusajili washambualiaji alisema

Haki miliki ya picha empics
Image caption 'hakuna haja, ya mshambulizi mpya sisi ni timu bora zaidi mara tatu' van Gaal

"hakuna haja, sisi ni timu bora zaidi mara tatu"

United walikosa nafasi tele kuchukua uongozi dhidi ya Newcastle, Bao la Rooney lilikatiliwa baada ya kupatikana kaotea huku jaribio la Chris Smalling kwa kichwa likiambulia patupu baada ya kugonga mwamba.

"Wayne alifunga ni vile tu haikuruhusiwa," aliongeza Van Gaal.

"Lakini pia ni mpira wa miguu nilivyosema mara nyingi unahitaji vifaa zaidi ili kusaidia uamuzi wa refariii."

Image caption "Wayne alifunga ni vile tu haikuruhusiwa," aliongeza Van Gaal.

Akizungumza kuhusu ukosefu wa mabao, Van Gaal alisema:

"Wasiwasi ni kwamba lazima tutawale mpinzani wetu, na hivyo ndivyo tulifanya leo na pia dhidi ya Aston Villa, Tottenham and Brugge, nimetosheka na vile walivyocheza leo na si matokeo".

Hata hivyo, Manchester wamehusishwa na mshambulizi matata wa Barcelona Neymar, alipoulizwa Van Gaal alisema kuwa hatazungumzia swala hilo kwani ana jukumu la kujali maslahi ya wachezaji wake na timu yake ya Machester United.