West Brom 2-3 Chelsea 90''

Image caption Chelsea wanasajili ushindi muhimu wa mabao 3-2 dhidi ya West Brom ugenini.

Chelsea wanasajili ushindi muhimu wa mabao 3-2 dhidi ya West Brom ugenini.

Mabao ya Chelsea yalifungwa na kiungo mgeni kutoka Uhispania Pedro katika dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza.

Image caption Costa aliifungia chelsea bao la pili

Hii ndiyo iliyokuwa mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na 'the Blues'' katikati ya juma hili.

West Brom watajilaumu wenyewe baada yao kupoteza fursa ya kuilaza Chelsea mapema walipopoteza penalti.

Image caption James Morrison alipiga mkwaju hafifu na kipa Courtois hakufanya masihara nao

James Morrison alipiga mkwaju hafifu na kipa Courtois hakufanya masihara nao.

Courtois ambaye alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza tangu aoneshwe kadi nyekundu majuma mawili yaliyiopita alikuwa na kila sababu ya kutabasamu na kumfanya kocha Mourinho amsamehe kwa makosa yaliyopelekea yeye kutimuliwa.

Hata hivyo Diego Costa aliongezea matumaini ya the Blues kusahau kichapo walichopata majuzi alipofanya mambo kuwa mabao mawili kwa nunge kunako dakika ya 30.

Image caption César Azpilicueta

West Brom waliendelea kuuliza safu ya ulinzi ya Chelsea maswali na wakapata majibu kunako dakika ya 35 Morrison aliporekebisha makosa yake na kuifungia West Brom bao lao la kwanza.

César Azpilicueta alimhakikishia Mourinho alama zote tatu muhimu kwa bao lake la dakika ya 42.

James Morrison aliendelea kuwa mwiba katika safu ya ulinzi ya Chelsea .

Gonga gonga yake ilisababisha bao la pili kwa mkwaju wa kichwa.

Image caption Terry aoneshwa kadi nyekundu

West Brom waliendelea kufanya mashambulizi na shinikizo lao likasababisha Kiungo wa Chelsea John Terry kuoneshwa kadi nyekundu kwa kumburura Salomón Rondón.

Mwisho wa kuishia The Blues wanarejea darajani wakiwa wametia kibindoni alama tatu muhimu.

Chelsea wanasajili ushindi muhimu dhidi ya West Brom ugenini.

Mpira umekwisha.

90:02

West Brom 2-3 Chelsea ''

John Obi Mikel anaingia uwanjani kuchukua pahala pa Pedro

83:02

Freekick kwa upande wa Chelsea (Pedro)

82:13 West Brom 2-3 Chelsea

West Bromwich Albion wanajipatia kona Branislav Ivanovic.

Image caption Gary Cahill

70:13

Gary Cahill akiwa amevalia barakoa baada ya kujeruhiwa pua

Je uamuzi wa refarii Mark Clattenburg kutoa kadi nyekundu umekurithisha ?

Image caption Je uamuzi wa refarii Mark Clattenburg kutoa kadi nyekundu umekurithisha ?

65:28 West Bromwich Albion 1- 3 Chelsea

GOOOOOOOL

James Morrison anafungia West Brom bao la pili kwa kichwa

58:34West Brom 2-3 Chelsea

West Bromwich Albion 1- 3 Chelsea

Image caption Terry

53:21 John Terry (Chelsea) anaoneshwa kadi nyekundu

50:34

West Bromwich Albion 1- 3 Chelsea

46:41

Kona kuelekea lango la Chelsea

45:00 Pedro anaunawa mpira

Image caption West Bromwich Albion 1, Chelsea 3.

West Bromwich Albion 1, Chelsea 3.

Kipindi cha pili kimeanza

Kipindi cha kwanza kimekamilika hapa The Hawthorns

Matokeo ni West Bromwich Albion 1- 3 Chelsea

Image caption West Bromwich Albion 1- 3 Chelsea

45:00

West Bromwich Albion 1- 3 Chelsea

41:40 Goal scored

Goooooooooool!

Image caption Bao la tatu la Cesar Azpilicueta

West Bromwich Albion 1- 3 Chelsea

César Azpilicueta

30:00

West Bromwich Albion 0, Chelsea 2

Image caption West Bromwich Albion 0, Chelsea 2

29:01

GOOOOOOL Diego Costa anaifungia chelsea bao la pili West Bromwich Albion 0, Chelsea 2 ''

24:01

Image caption Courtois akiokoa penalti

West Brom 0-1 Chelsea

19:30

GOOOOOOOOAL

Pedroooooo

Pedro akifungua akaunti yake Chelsea

West Brom 0-1 Chelsea

Image caption Courtois

17:45 West Brom 0-0 Chelsea

Freekick kuelekea lango la Chelsea

Callum McManaman (West Bromwich Albion) anachezewa visivyo

16:11

Nemanja Matic (Chelsea) anaoneshwa kadi ya njano

12:35 LOOOOOOO

Penalti inaokolewa hapa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Courtois ameokoa penalti

Amini usiamini James Morrison wa West Bromwich Albion anapiga mpira hafifu na kipa nambari moja Courtois anathibitisha kwanini yeye ndiye anayepewa majukumu langoni

12:27 Penalti kuelekea lango la Chelsea

Nemanja Matic anacheza visivyo

5:03 West Brom 0-0 Chelsea

Image caption Mechi imeanza

Diego Costa anafanya mashambulizi ya mapema mbele ya lango la wenyeji wao

3:21

West Brom v Chelsea

Image caption Kocha Tony wa West Brom

Salomón Rondón wa West Bromwich Albion anamjaribu kipa wa Chelsea Courtios

Mechi imeanza kwa kishindo

Image caption Timu ya West Brom

West Bromwich Albion

13 Myhill 25 Dawson 23 McAuley 03 Olsson 11 Brunt 24 Fletcher 05 Yacob 19 McManaman 14 McClean 07 Morrison 33 Rondón

Image caption Mashabiki wameanza kuwasili hapa uwanjani

Wachezaji wa akiba

04 Chester 06 Lescott 08 Gardner 10 Anichebe 17 Lambert 31 Gnabry 38 Rose

Image caption Timu ya Chelsea

Kikosi cha Chelsea;

13 Courtois 02 Ivanovic 26 Terry 05 Zouma 28 Azpilicueta 04 Fàbregas 21 Matic 17 Pedro 22 Willian 10 Hazard 19 Diego Costa

Wachezaji wa akiba

Image caption Pedro aliyesajiliwa majuzi na Chelsea

01 Begovic 09 Falcao 12 Mikel 14 Traore 18 Remy 24 Cahill 36 Loftus-Cheek

Victor Moses na Oscar, hawatakuwa uwanjani baada ya kuripotiwa kujeruhiwa mazoezini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bila shaka Kocha Jose Mourinho angependa kusahau matokeo ya mechi yao ya mwisho

Kocha Jose Mourinho anajivunia kiungo mpya Pedro

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kocha Mourinho

Chelsea wanahitaji ushindi kwa udi na uvumba ilikufufua kampeini yao msimu huu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kikosi cha utabibu cha Chelsea

Bila shaka Mourinho angependa kugonga vichwa vya Habari kwa kushinda wala sio kutofautiana na kitengo cha utabibu

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kipa Courtois aliyeonesha kadi nyekundu anarejea uwanjani leo

Karibu katika matangazo ya moja kwa moja kati ya West Brom na Chelsea.