Barcelona waanza kwa ushindi

Mabingwa watetezi Barcelona wameanza msimu mpya wa ligi ya Hispania baada ya kuishinda Athletic Bilbao kwa bao moja kwa bila.

Nao wapinzani wao Real Madrid wamejikuta wakianza kwa kupepesuka baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana walipocheza dhidi ya Sporting de Gijon, huku Villarreal ikikabwa koo na Real Betis kwa kutoka sare ya bao 1-1