Monaco na Celtic nje Klabu bingwa Ulaya

Image caption Wachezaji wa timu ya Valencia

Usiku wa kuamkia leo timu kadhaa za soka barani Ulaya zilishuka dimbani kutafuta tiketi ya kufuzu kuingia katika hatua ya makundi kwenye mashindano ya klabu bingwa barani humo.

Monaco ya Ufaransa, walikuwa nyumbani kucheza dhidi ya Valencia. Hadi mwisho wa mchezo huo Monaco imeibuka kidedea kwa jumla ya bao 2-1.

Hata hivyo Valencia imefuzu hatua ya makundi kwa jumla ya bao 4-3, baada kushinda bao 3-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza. Nayo Malmo FF ikaiadhibu Celtic kwa jumla ya bao 2-0, na kusonga mbele kwa jumla ya bao 4-3.

Mechi hizo zitaendelea leo hii kwa timu kadhaa kushuka dimbani. Manchester utd itakua ugenini kucheza dhidi Club Brugge, huku Bayer Liverkusen itamenyana na Lazio. CSKA Moscow itakipiga dhidi ya Sporting Lisbon.