Farah afuzu fainali za mbio za 5000m

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bingwa mtetezi Mo Farah aliye na umri wa miaka 32

Mwanariadha wa Uingereza Mo Farah aliyeshinda taji lake la sita duniani aliposhinda dhahabu kwa mbio za mita 10,000 mwishoni mwa juma, amefanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili katika muda wa dakika 13:19.44.

Bingwa huyo mtetezi aliye na umri wa miaka 32 aliguswa mgongoni na mwanariadha wa Canada Mohammed Ahmed lakini hatimaye alifanikiwa kukimbia imara.

Mwanariadha mwenza kutoka Uingereza Tom Farrell aliibuka katika nafasi ya nne kufuzu pia katika fainali hiyo.

Ahmed alikuwa wa tatu lakini awali alipigwa marufuku na maafisa, na baadaye kurudishwa baada ya kulalamika.

Haki miliki ya picha
Image caption Mo Farah ameshinda taji lake la sita duniani kwa mbio za mita 10,000

"Nina bahati sikuanguka, ningelianguka tena," Farah, ambaye karibu aanguke tena katikati mwa mbio hizo aliiambia BBC Sport.

"Wakati huo ni lazima uwe imara, na uwe na umakini."

Farah ameongeza kwamba alikuwa akiumwana mguu lakini akaongeza kwamba "sio jambo la kutia wasiwasi".

Alikabiliwa na mkasa kama huo miaka 7 iliyopita katika uwanja huo na kutoka katika mashindano ya olimpiki baada ya kushindwa kufuzu kwa fainali za 5,000m.

Lakini sasa atashindana mara moja tena kabla ya kujinyakulia ushindi mara mbili baada ya kushinda dhahabu kwa mbio za mita 5,000 na 10,000 huko London 2012 na 2013 katika mashindano ya dunia Moscow.