Asbel Kiprop afuzu kwa fainali-Beijing

Wanariadha wanne wa Kenya wamefuzu kwa fainali ya mbio za mita 1500 kwa upande wa wanaume, katika mashindano ya riadha ya Dunia yanayoendelea mjini Beijing.

Bingwa mtetezi Asbel Kiprop alimaliza wa katika katika kundi la kwanza kwa kutumia muda wa dakika 3.43.48, akifutawa na Nicholas Willis wa New Zeland and Silas Kiplagat.

Mshindi wa medali ya fedha katika mashindano yaliyopita Mathew Centrowitz WA Marekani pia alifuzu kwa fainali.

Katika kundi la Pili, Elijah Motonei na Timoth Cheruiyot walifuzu kwa fainali hizo. Motonei aliandikisha muda wa kasi zaidi katika awamu hiyo ya nusu fainali kwa kutumia muda wa dakika 3.35.00.

Wanariadha wengine wa Afrika waliofuzu kwa fainali hizo za mita 1500 ni pamoja Tapufik Makhloufi wa Algeria, Abdalaati Iguider wa Morocco na Aman Wote wa Ethiopia.