Arsenal, Bayern kundi moja UEFA

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Arsenal wanakutana tena na Bayern Munich

Baada ya jana kufanyika droo ya makundi ya klabu bingwa barani Ulaya, mashabiki wa soka watapata fursa ya kushuhudia baadhi ya historia zikijirudia huku zingine mpya zikiandikwa.

Arsenal kwa mara ya tatu katika misimu minne, itavaana na Bayern Munich baada ya kupangwa kundi moja.

Wakati hayo yakijiri, mchezaji mpya wa Manchester Utd Memphis Depay atapata fursa ya kupambana na timu yake ya awali ya PSV Eindhoven ya uholanzi baada ya timu hizo kupangwa kundi moja.

Na ligi kuu ya Hispania La liga, pia mwaka huu imeweka historia baada ya mwaka huu kuingiza timu tano katika hatua hiyo ya makundi, jambo ambalo halikuwahi kutokea hapo awali.

Timu hizo ni Real Madrid, Barcelona, Atletico Madrid, Valencia pamoja na Sevilla.