Nigeria mabingwa wa Afrika mchezo wa vikapu

Image caption Angola wakicheza na Tunisia

Nigeria imeishinda Angola alama 74 kwa 65 katika fainali ya mashindano ya Bara la Afrika ya Afrobasket ya mwaka huu yaliyofanyika nchini Tunisia na kujinyakulia taji lao la kwanza kwenye mashindano hayo.

Haki miliki ya picha FIBAAFRICA
Image caption Nigeria kwenye fainali

Ushindi huo walioupata siku ya Jumapili umeipa Nigeria tikiti ya kushiriki katika michezo ya Olimpiki itakayo andaliwa mjini Rio nchini Brazil mwaka ujao.

Angola, Tunisia iliyomaliza katika nafasi ya tatu na Senegal iliyomaliza katika nafasi ya nne pia zimejikatia tikiti ya kuelekea mjini Rio kwa michezo ya Olimpiki.