Maria Sharapova kuikosa US Open

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Nyota na tatu mchezo wa Tenisi duniani, Maria Sharapova

Nyota namba tatu wa mchezo wa Tenesi duniani kwa upande wa wanawake Maria Sharapova amejitoa kushirikia michuano Us Open.

Sharapova amejiondoa katika michuano hiyo ya wazi kwa sababu ya kusumbuliwa na maumivu.

Nyota huyu mwenye miaka 28 hajashuka dimbani tangu ilipomalizika michuano ya Wimbledon,ambapo aliumia goti.

kupitia ukurasa wake wa Facebook, ameandika "Nimefanya kila ninachoweza kuwa tayari lakini muda hautoshi."

Daria Kasatkina wa Urusi amechukua nafasi ya Sharapova katika kusaka nafasi za kufuzu kama best loser.