Uhamisho wa De Gea wakwama

Image caption Golikipa wa Manchester United, David De Gea

Uhamisho wa Golikipa David De Gea kutoka Manchester United kwenda Real Madrid ya Hispania umekwama dakika za mwisho kwa sababu ya karatasi muhimu za uhamisho kuchelewa .

Madrid walikua tayari kutoa dau la pauni milioni 29 , kipa wao Keylor Navas kama sehemu ya dili la uhamisho huo.

Hakujakua na taarifa rasmi kutoa kwa vilabu hivi ni nini kimetokea juu ya uhamisho huo huku dirisha la usajili kwa nchi ya hispania likifugwa jana na kwa upande wa Uingereza litafungwa leo hii sasa sita usiku.

Kusalia kwa De Gea kunaifanya Man United kuwa na makipa wanne ambao ni Sergio Romero,Victor Valdezna kinda Sam Johnstone.