Taifa Stars kurejea leo toka Uturuki

Image caption Timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa stas

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajiwa kurejea leo usiku kutoka nchi Uturuki ilikokua imeweka kambi .

Taifa Stars iliweka kambi ya wiki moja kujifua na mchezo wake dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria hapo Septemba 5, 2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika mwaka 2017.

Kocha Mkuu wa Stars Charles Mkwasa akiongea na tovuti rasmi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) anasema kambi imekwenda vizuri na wachezaji wanaonyesha mabadiliko makubwa sana.

Mara baada ya kuwasili timu itaendelea na kambi kwa kufanya mazoezi mepesi siku ya jumatano pamoja wa wachezaji wa kimataifa Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngasa katika uwanja wa Taifa kujiandaa na mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya Nigeria.