Usajili England wagharimu fedha nyingi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kocha wa Chelsie, jose Mourinho

Siku ya mwisho kwa dirisha la usajili wa ligi kuu ya England imekua na matumizi makubwa ya pesa. kama ilivyokua kwa usajili wa Robinho au Fernando Torres.

Ingawa usajili huu unagharimu fedha nyingi, lakini mara nyengine huchukua muda kuzaa matunda.Lakini mara hii, kulikuwa mparaganyiko kuhusu mikataba ambayo haikufanikiwa kuliko ile ambayo imefanikiwa.

Kwanza, ambayo haikufanikiwa, ni kwa mabingwa wa Chelsea, kwa kuanza kampeni hii kwa kuwa na safu ya ulinzi dhaifu, wakiwa wamewasajili walinzi Papy Djilobodji na Michael Hector.Kwa kufanya hivyo wamelazimika kuwatoa wachezaji 33 kwa mkopo ,ikiwa ni zaidi ya vilabu vingine vyote vya ligi kuu.

Kumekua na usajili mkubwa kwa timu za kati Everton na Southampton kwa walinzi Ramiro Funes Mori na Virgil van Dijk kujiunga na timu hizo za Goodison na St Mary's.

Kwa upande mwingine Manchester United wamefanya usajili wa kushangaza, sio kwa usajili huu tu bali kushinda dirisha lingine lolote la usajili kwa kutumia pauni milioni 36 kumsajili kinda Anthony Martial kutoka Monaco, ambae amecheza michezo 52 ya ligi na kufunga mabao 11.

Martial amekua akifananishwa na nyota wa zamani wa timu ya taifa ya ufaransa Thierry Henry, wote wakiwa na uwezo wa kuumiliki mpira na kuuchezea huku wakiaanzia kutengeneza majina yao katika klabu ya Monaco.

Kama Manchester United watapa kile alichokifanya Henry kwa Arsenal kutoka kwa Martial, basi dau la pauni milioni 36, litakuwa limetumika sahihi. Henry anabaki kuwa mmoja kati ya wachezaji bora wa kihistoria wa ligi kuu ya England.

Haki miliki ya picha PA
Image caption mouriinho akiwa na Arsene Wenger

Hata hivyo, Henry alikuwa mkubwa kidogo na alipewa muda zaidi kukua wakati huo Ian Wright alikuwepo bado kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Arsenal.

Lakini kwa United walioruhusu kuondoka kwa Angel di Maria, Javier Hernandez, Radamal Falcao na Robin van Persie katika majira ya joto, shinikizo litakua kwa Martial kuhalalisha thamani ya dau lake la usajili mapema sana.

Na halikua dili pekee lilitokea hapo Old Trafford watu wamekua wakijiuliza juu ya ujuzi wa kocha Louis van Gaal katika dirisha la usajili.

Kwa sababu ya kivuli cha usajili wa siku nzima, ulioshindikana wa golikipa David de Gea kwenda Real Madrid huku kipa wa Costa Rica Keylor Navas akija upande wa pili.

Kilichotokea katika usajili wa saa nane, maafikiano yalifikiwa na karatasi za usajili zikatumwa pengine bila kujulikana. Real Madrid wanasema halikua kosa lao huku United wakisisitiza walifanya kila kitu kwa muda sahihi.

Chochote, ni aibu kwa wote wanaohusika. na van Gaal kwa sasa anakwama kwa kipa ambaye ni wazi ni moja kati ya makipa bora duniani, hataki kuwa huko na thamani yake inazorota kila siku pamoja na mkataba wake anaendesha mwishoni.

Katika uhamisho wa kujutia ni wa mshambuliaji chipukizi wa timu taifa ya England Saido Berahino, ambae kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ameandika. "Kamwe siwezi kucheza kwa mara ya pili chini ya mwenyekiti Jeremy Peace baada ya kukataa mara nne ofa za Tottenham kwa ajili usajili wa Berahino."

Berahino alikua na matumaini ya kushinikiza kwa amani mpango wa kuhama katika dakika za mwisho kabla dirisha la usajili kufungwa. Ila ikashindikana.

Berahino tayari alikua anajua hawezi kuwa mashuhuri katika chumba cha kubadilishia nguo cha klabu ya West Brom hatua hii itakuwa kwa yeye na wachezaji wenzake, na wakati anarejea klabuni asubuhi kuna uwezekano wa kutafiri upya neno.

Pia Tottenham inaonekana dhaifu kwenye safu ya ushambuliaji huku kukiwa hakuna mtu wa kumsaidia Harry Kane.

Na huko kaskazini mwa London, Arsenal walikua sawa huku wakionekana kukosa bahati ya mchezaji wa kumsajili.

Lakini dili kama la Martial, linaonyesha namna mbinu za usajili zinaweza kupandisha dau.

Baada ya yote, ina maana bado tena kuna rekodi kwa Ligi Kuu ya kutumika kwa $ 1.33bn (£ 863m) mpaka muda unamalizika.

Kama usajili wa De Gea na Berahino, ungefanikiwa kiasi hicho cha pesa kingefikia jumla zaidi ya £900m.

Mwaka ujao, wakati sehemu ya kwanza ya malipo mapya, tutaona £ 1bn zikitumika katika dirisha la usajili.