Nadal atolewa nje ya Michuano ya US Open

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rafael Nadal

Bingwa namba nane kwa ubora duniani katika mchezo wa tenis Rafael Nadal ametolewa nje ya mashindano ya tenis ya US Open huko Marekani baada ya kukubali kipigo kutoka kwa mpinzani wake Fabio Fognini.

Fognini ambaye ni bingwa namba 32 kwa ubora duniani alimshinda Nadal kwa seti 3-6 4-6 6-4 6-3 6-4.

Bingwa huyo wa Grand Slam mara 14 na bingwa wa US Open mara mbili alishinda seti mbili na kushindwa seti tatu.