Murray atinga 16 bora

Haki miliki ya picha AP
Image caption Andy Murray

Andy Murray atinga hatua ya 16 bora kwa kumfunga Thomaz Bellucci katika michuano ya US open inayoendelea nchini Marekani.

Muingereza Andy Murray amepata mafanikio mepesi katika michuano ya US Open mnamo raundi ya nne baada ya kumcharaza mfululizo Mbrazili Thomaz Bellucci.

Murray alikuwa akihitaji seti tano kushinda duru yake ya awali lakini kwa ushindi wa seti 6-3 6-2 7-5 mjini New York ulifanya mambo yawe mepesi kwake.

Kwa ushindi huo atakipiga dhidi ya Kevin Anderson wa Afrika ya Kusini katika hatua ya kumi na sita bora siku ya jumatatu.