Kucheza Jumamosi kwazua mvutano Israel

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Timu ya taifa ya Isreal

Mamlaka ya soka nchini Israel imesimamisha mipango ya mgomo katika mzozo kuhusu kucheza siku ya Sabato ya Wayahudi.

Uhalali wa mechi za Jumamosi umetiliwa shaka na Mahakama ya kazi ya Israel,ambayo imekuwa ikiwaunga mkono wachezaji wayahudi juu ya madai yao.

Lakini chama cha soka cha Israel kimesema kuwa michezo yote itaendelea kama ilivyopngwa baada ya mwanasheria mkuu kuthibitisha kuwa hakuna mtu ambaye atafunguliwa mashitaka.