Rooney avunja rekodi ya magoli England

Haki miliki ya picha PA
Image caption Wayne Rooney

Wayne Rooney ameivunja rekodi ya upachikaji mabao ya muda wote katika timu ya taifa ya England, iliyokuwa ikishikiliwa na Sir Bobby Charlton katika mchezo dhidi ya Switzerland,uliopigwa uwanjani Wembley wa kufuzu kwa michuano ya ulaya mwaka 2016.

Nahodha huyo wa England aliifikia rekodi ya Charlton ya magoli 49,wakati alipofunga dhidi ya San Marino siku ya Jumamosi.

Alikua pia katika mchezo dhidi ya Switzerland siku ya Jumanne ambapo alifikisha goli la 50 na kufuta historia hiyo iliyodumu kwa miaka 45.