Man U yamrudia tena De Gea

Haki miliki ya picha Getty
Image caption David De Gea

Manchester United imeanza mazungumzo ya mkataba mpya na mlinda mlango wake David De Gea.

Mkataba wa sasa na Muhispaniola huo unafikia ukingoni mwaka 2016 na United wameonyesha matumani ya kurefusha muda wa De Gea kutumika ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi hii ikitokana na mipango ya De Gea kutimkia kunako klabu ya Real Madrid kukwama.

Manager Louis van Gaal hakumtumia mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid mpaka dirisha la usajili lilipofungwa kwa vile hakukuwa na uhakika juu ya mustakabali wake.

Bado haijajulikana kama De Gea ataanza katika mchezo wa jumamosi wa Ligi ligi dhidi ya Liverpool.