Michuano ya ACL kuingia nusu fainali

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wachezaji wa Al Hilal

Michuano ya kuwania kombe la klabu bigwa barani Afrika kufika hatua ya nusu fainali hiyo kesho.

Katika kundi la A, mabingwa mara nne wa kombe hilo TP Mazembe, kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Al Hilal ya Sudan, Moghreb Tetouan ya Morocco watajibwaga uwanjani kutafuta nafasi ya kuingia fainali.

Timu hizi tatu zina rekodi sawa ya kushinda mechi mbili kila mmoja, zimetoka sare mechi mbili na kushindwa mechi moja.

Hii inamaanisha kuwa timu hizo sasa zitaorodheshwa kwa mujibu wa mechi walizocheza pamoja Tetouan ikiwa ya kwanza ikifuatwa na Hilal nayo TP Mazembe ikiwa ya tatu.

Ratiba ya siku ya Jumamosi

  • Smouha v Al Hilal
  • TP Mazembe v Moghreb
Image caption Wachezaji wa TP Mazembe

Lakini kati yao TP Mazembe ndiyo itakayokuwa ikicheza katika uwanja wao wa nyumbani hiyo kesho dhidi ya Tetouan katika uwanja wa Stade Kamalondo, iliyoko eneo la Kusini lenye utajiri mkubwa wa madini wa Lubumbashi.

Hilal, itakuwa ikipania kujiunga na Al Merrikh iliyo na makao yake mjini Omdurman katika semi fainali na itakwaruzana na Smouha ya Misri ambayo tayari imepoteza mechi zake nne.