Martina , Sania mabingwa wa tenesi

Image caption Martina Hingis na Sania Mirza, mabingwa Tenisi wanawake

Martina Hingis na Sania Mirza, wametwaa ubingwa wa michuano ya wazi ya Us Open kwa upande wa wachezaji wawili wawili wanawake.

Ushindi huu ni wa nne kwa mwaka huu kwa wachezaji hawa huku ukiwa ni ushindi wao wa pili wa Grand Slam .

Nyota hawa waliwashinda wapinzani wao Yaroslava Shvedova na Casey Dellacqua kwa seti 6-3 6-3.

Hingis mwenye miaka 34 alishinda taji la mchanganyiko kwa wachezaji wawili wawili na kumpelekea kutwaa vikombe vitano kwa mwaka huu wa 2015.