Voliboli: Wanawake wa Kenya vinara

Image caption Timu ya Voliboli ya Wanawake Kenya

Timu ya taifa ya wanawake ya mchezo wa voliboli wametwaa ubingwa wa mchezo voliboli katika michezo ya All Africa games.

Kenya waliwashinda wapinzani wao Cameroon kwa seti 3 kwa 1 seti ya kwanza kenya walipoteza kwa 15-25 kisha wakapata ushindi kwa 25-14/25-15/25-19

Huu ni ushindi wa kwanza katika kwa timu hiyo katika mchezo wa fainali toka mwaka 1999 katika michuano hiyo ya Afrika.

Kocha wa kikosi hicho Paul Gitau amekipongeza kikosi chake kwa kucheza kwa ushirikiano kama timu.