Ligi kuu Tanzania bara kuendelea leo

Image caption Kikosi cha klabu ya soka, Yanga ya Tanzania

Ligi Kuu Tanzania bara Itaendelea tena leo katika viwanja saba ikiwa ni michezo ya mzunguko wa pili.

Mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Young Africans watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,

Maafande wa Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa Simba SC katika dimba la uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Wana Lizombe Majimaji ya mjini Songea watawakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

jijini Mbeya watoza kodi wa jiji timu ya Mbeya City watawakaribisha maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Ruvu katika uwanja wa Sokoine.

Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Stand United watakuwa wenyeji wa timu ya Azam FC, Toto Africans watawakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Coastal Union kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.