Bondia afariki baada ya 'knock out'

Image caption David Browne

Mwana masumbwi mmoja wa Australia amefariki siku nne baada ya kupoteza fahamu alipopigwa 'knock out' katika pigano la kijimbo mjini Sidney.

Davey Browne mwenye umri wa miaka 28 aliangushwa na Carlo Magali wa taifa la Ufilipino mwisho wa raundi ya 12 katika taji la uzani wa Feather siku ya Ijumaa.

Brown ambaye ni baba ya watoto wawili alipelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya mitambo inayomsadia kuzimwa alipokosa kuimarika kiafya.

Muungano wa wahudumu wa matibabu nchini Australia umetaka mchezo wa ndondi kupigwa marufuku nchini humo kufuatia kifo hicho.

Kifo cha Browne kinajiri wiki sita baada ya mwanamasumbwi wa Queensland Braydon Smith kuzirai na kufariki kufuatia pigano la uzani wa Feather nyumbani kwake huko Toowoomba.