Chelsea 2-0 Arsenal

Mpira umekwisha.

ChelseaFC 2-0 Arsenal

Kufuatia ushindi huu Chelsea sasa wamepanda hadi nafasi ya 10 katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza.

Arsenal wamesalia katika nafasi ya nne japo sasa wamo katika hatari ya kushuka iwapo wataendelea kupata matokeo kama haya.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hazard

4:36 ChelseaFC 2-0 Arsenal

GOOOOOOOOOOAL

@ChelseaFC 2-0 @Arsenal Eden Hazard 90''

Hazard anaupiga lakini wapi unakuwa mwingi na kutoka nje na kuwa ni Kona

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Fabregas

Kona kuelekea lango la Arsenal

Fabregas ndiye anayeupiga

Freekick kuelekea lango la Arsenal nje tu ya eneo la lango

Kocha Jose Mourinho amesalia na dakika 10 tu kusajili ushindi wake wa pili katika ligi kuu ya Uingereza

Haki miliki ya picha PA
Image caption Makocha hao mahasidi wakizomeana uwanjani

Wapinzani wake Arsenal wamesalia 9 uwanjani.

Diego Costa anaondoka uwanjani anapumzika

Japo hakufunga bao, ndiye aliyechangia pakubwa kwa idadi ya wachezaji Arsenal kupungua uwanjani

4:24 ChelseaFC 1-0 Arsenal

Refarii Mike Dean anatoa kadi ya pili nyekundu dhidi ya mchezaji wa Arsenal Carzola

Arsenal wamesalia wachezaji 9 uwanjani.

Hazard anakosa

Hazarddddddddd !

Lo !

4:07 ChelseaFC 1-0 Arsenal

Haki miliki ya picha ALLSPORT Getty
Image caption Sancheza anapoteza nafasi nzuri ya kusawazisha dhidi ya Chelsea

Kurt Zouma anaifungia Chelsea bao muhimu dhidi ya Arsenal kunako dakika ya 52 ya mechi hii

GOOOOOOOOAL

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kurt Zouma anaifungia Chelsea bao muhimu dhidi ya Arsenal kunako dakika ya 52 ya kipindi cha pili

3:57 ChelseaFC 1-0 Arsenal

Haki miliki ya picha Getty

3:50 ChelseaFC 0-0 Arsenal

Kipindi cha pili kimeanza

Chelsea wakiwa na nguvu ya mtu mmoja zaidi wanawashambulia wapiga bunduki mapema

3:35 ChelseaFC 0-0 Arsenal

ChelseaFC 53% - 47% Arsenal

Image caption Arsenal wamesalia 10 uwanjani kwa mara ya pili katika juma moja

Kipindi cha kwanza kimekamilika bila ya bao lolote.

Arsenal hata hivyo watalazimika kubadili mipango kwani watakosa huduma za Gabriel katika kipindi cha pili.

3:35 ChelseaFC 0-0 Arsenal

Hii ni mara ya pili katika juma moja ambapo Arsenal wanajipata bila mchezaji mmoja uwanjani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Diego Costa anashambulia lango la Arsenal

Gabriel wa Arsenal anaoneshwa kadi Nyekundu.

Refaree Mike Dean anamuonesha kadi nyekundu kwa kuzozana na Mshambulizi wa Chelsea Diego Costa

3:29 ChelseaFC 0-0 Arsenal

Arsenal wanapoteza nafasi nzuri ya kufunga bao la kwanza

Sasa Chelsea wanashambulia

3:19 ChelseaFC 0-0 Arsenal

Diego Costaaaaaa

Costa anapoteza nafasi nyengine ya wazi

Kwa hakika Chelsea inafanya mashambulizi kwenye lango la Arsenal

3:11 ChelseaFC 0-0 Arsenal

Image caption ChelseaFC 0-0 Arsenal

Diego Costa anashambulia lango la Arsenal

Diego Costaaaaaa

Tutumie ujumbe wako kupitia mtandao wa twitter

Tafuta BBCSwahili

kama msomaji wetu huyo Anjesco

Wapi,,,,,

Image caption ChelseaFC 0-0 Arsenal

Kipa nambari moja Peter Cech anaupakata mkwaju wa Costa

3:05 ChelseaFC 0-0 Arsenal

Nipe nikupe kati ya hazard na Costa nusura izae matunda

Lakini wapi

3:02@ChelseaFC 0-0 @Arsenal

2:57 '' @ChelseaFC 0-0 @Arsenal

Haki miliki ya picha PA
Image caption Sanchez

Hatimaye Wenger alikubali salamu za mwenyeji wake Mourinho

Arsenal wanafanya mashambulizi ya mapema kuelekea lango la Wenyeji wao

2:53 ''Chelsea 0-0 Arsenal

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Diego Costa

Arsenal wanapata Kona ya kwanza

Konaaaa kuelekea upande wa Chelsea

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mourinho na wachezaji wake

2:45 Mpira umeanza !

Chelsea 0-0 Arsenal

Branislav Ivanovic anaiongoza Chelsea kuingia uwanjani Stamford Bridge.

John Terry leo hayuko

Leo anapasha benchi moto

Je hii ni dalili kuwa uhusiano wake na kocha Mourinho umezorota?

Kikosi cha Arsenal

33 Cech 24 Bellerín 05 Gabriel 06 Koscielny 18 Monreal 34 Coquelin 19 Cazorla 16 Ramsey 11 Özil 17 Sánchez 14 Walcott

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mourinho amekanusha uvumi kuwa ametofautiana na John Terry

Wachezaji wa Akiba

02 Debuchy 03 Gibbs 08 Arteta 12 Giroud 13 Ospina 15 Oxlade-Chamberlain 21 Chambers

Image caption Stamford Bridge

Kikosi cha Chelsea

01 Begovic 02 Ivanovic 24 Cahill 05 Zouma 28 Azpilicueta 04 Fàbregas 21 Matic 17 Pedro 08 Oscar 10 Hazard 19 Diego Costa

Wachezaji wa Akiba

07 Ramires 09 Falcao 12 Mikel 18 Remy 26 Terry 27 Blackman 36 Loftus-Cheek

Image caption Chelsea

Kocha mbishi Jose Mourinho amemuonya mwenzake wa Arsenal, kuwa timu yake imerejesha makali yake na kuwa mechi ya leo huko darajani ama ukipenda Stamford Bridge itakuwa kiziba mkonga tu ya uamko mpya.

Hayo yanajiri magwiji hao wawili wakitokea kwenye kidumbwedumbwe cha kombe la mabingwa barani ulaya ambapo 'the Blues' walipata ushindi mkubwa wa mabao 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv.

Haki miliki ya picha PA

Arsenal kwa upande wao walipigwa mabao mawili kwa moja mikononi mwa Dinamo Zagreb.

Licha ya usemi huo, Chelsea itakosa huduma za mshambulizi wake wa kati kati Willian kutokana na jeraha alilopata katika mechi hiyo ya katikati ya wiki.

hamstring .

Radamel Falcao, Oscar na Pedro huenda wakacheza ama wasicheze.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mbivu na mbichi kubainika leo Arsenal wanapoitembelea Chelsea Stamford Bridge

kwa upande mwengine,kipa nambari moja Petr Cech, atarejea katika uwanja anaoufahamu vyema tu wa Stamford Bridge baada ya kushuhudia kichapo dhidi ya Zagreb kutoka mbali.

Haijabainika iwapo Per Mertesacker atarejea baada ya kuugua kwa kipindi kirefu.

Kufikia sasa Arsenal, wanashikilia nafasi ya 4 katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza wakiwa wamecheza mechi 5 wakajishindia alama 10.

Chelsea kwa upande wao wanashikilia nafasi ya 17 wakiwa wamecheza mechi 5 na kujizolea alama 4 pekee.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mbivu na mbichi kubainika leo Arsenal wanapoitembelea Chelsea Stamford Bridge

Chelsea wameshinda mechi moja pekee kufikia sasa.

Je mechi hii itakuwa na tofauti kwao ?

Ungana name katika matangazo ya moja kwa moja kati ya Chelsea na Arsenal.