Southampton 2- 3 Manchester United

Mshambulizi mpya wa Manchester United, Anthony Martial alithibitisha thamani yake alipoiongoza timu yake kusajili ushindi muhimu wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya wenyeji wao Southampton.

Martial alijiunga the red devils kwa kitita cha pauni milioni 36 .

Man United walianza vibaya mechi hii na kuwaruhusu The saints kupata bao la mapema kupitia kwa Graziano Pelle.

Image caption Martial akimsaidia mpinzani wake Virgil van Dijk

Pelle alifuma kimiani mkwaju uliokuwa umetemwa na kipa wa United, David De Gea kunako dakika ya 13.

Hata hivyo Martial aliisawazishia United.

Martial hakukuwa amemalizana nao,

Image caption Mpira umekwisha na United wanarejea nyumbani na alama 3 muhimu

Alimpa kocha van Gaal sababu ya kutabasamu baada ya kutumia vyema makosa ya Maya Yoshida aliyemega mpira hafifu kurudi nyuma kwa mlinda lango naye akaufyatua kimiani.

Juan Mata alifunga bao la tatu dakika chache tu kabla ya Pelle kufunga bao lake na la pili na la Southampton.

Image caption Graziano Pellè anaifungia Southampton bao la pili

Vijana wa Louis van Gaal waliandikisha ushindi wao wa pili mfululizo baada ya kuibana Liverpool juma lililopita.

Kufuatia ushindi huo united wameimarika hadi kushika nafasi ya pili katika ligi ya EPL nyuma ya mahasimu wao manchester City.

Southampton imeshinda mechi mbili pekee baada ya kucheza mechi 12.

90:00 +5:20 Mpira umekwisha.

Southampton 2-3 Manchester United

Manchester United wanasajili ushindi muhimu dhidi ya Southampton

Image caption De Gea

Kufuatia ushindi huu muhimu vijana wa van Gaal wanakwea hadi nafasi ya pili katika jedwali la EPL.

90:00 +4:20 Freekick

Anthony Martial (Manchester United)

Southampton wanafanya mashambulizi dakika za lala salama .utadhani ndio wamegutuka kutoka usingizini !

90:00 +1:53 Kona

Image caption Southampton wanafanya mashambulizi dakika za lala salama .utadhani ndio wamegutuka kutoka usingizini !

Southampton

David de Gea anapangua mkwaju wa Wanyama.

90:00 +1:53 Southampton 2-3 Manchester United

Wanyamaaaaaaaa !

wapi

David de gea anafanya kweli

85:27

GOOOOOOOOOOAL

Southampton

Southampton 2-3 Manchester United

Graziano Pellè anaifungia Southampton bao la pili

Image caption Southampton hawaamini kilichotokea hapa

78:58 Offside, Manchester United Memphis Depay ameotea

Southampton 1-3 Manchester United

Image caption Martial

77:11 free kick

Anthony Martial (Manchester United)

Image caption Furaha iliyoje kwa Mata ?

Southampton 1-3 Manchester United

75:42 free kick

Image caption Wanyama

Bastian Schweinsteiger (Manchester United)

72:27 free kick

Anthony Martial (Manchester United)

Image caption Bao la tatu la Mata

67:45 GOOOOOOOOAL

Southampton 1-3 Manchester United

Juan Mata anaifungia Manchester United bao la tatu

67:43

Memphis Depay (Manchester United) anagonga mchuma naye Bastian Schweinsteiger akijaribu bahati yake .

Anthony Martial anaisaidia Manchester kukwea hadi nafasi ya pili ya jedwali la ligi kuu ya EPL

Hili litawezekana iwapo wataibuka washindi wa mechi hii.

59:49

De Gea amelazimika kufanya kazi ya ziada hapa kuzuia bao la pili la Southampton

Badiliko

Manchester United wanamtoa Michael Carrick anaingia Bastian Schweinsteiger .

Image caption De Gea amelazimika kufanya kazi ya ziada hapa kuzuia bao la pili la Southampton

55:51 Kona Southampton

Image caption Kipindi cha pili kimeanza hapa

Kona kuelekea lango la Man united. (Marcos Rojo)

49:34 GOOOOOOAL

Anthony Martial anaifungia Man United bao la pili

Southampton 1-2 Manchester United

Image caption Bao la Southampton

Kipindi cha pili kimeanza hapa @SouthamptonFC 1 - 1 @ManUtd #SOUMUN

Southampton 1-1 Manchester United

Southampton 37%-63% Manchester United

Image caption Southampton 37%-63% Manchester United

45:00+ 1

Kipindi cha kwanza kimekamilika

Southampton 1-1 Manchester United

44:31 Mpira umesimamishwa ili Matt Targett (Southampton) atibiwe

Image caption Southampton 1-1 Manchester United

41:31 Kona,

Manchester United wanapata kona nyengine hapa baada ya Graziano Pellè kuutoa mpira.

40:37 Kona kuelekea lango la Southampton

Virgil van Dijk.

Image caption Makocha wawili wakiamkuana

Southampton 1-1 Manchester United

39:37 Offside, Manchester United.

Marcos Rojo anatuma pasi safi lakini mfungaji bao Anthony Martial ameotea

33:58 Southampton 1-1 Manchester United

Anthony Martial (Manchester United)

29:00 Southampton 1-0 Manchester United

28:56 free kick

Victor Wanyama (Southampton)

Southampton 1-0 Manchester United

Iwapo Manchester watajifurukuta na washinde mechi hii wataimarika hadi nafasi ya 2 katika jedwali la ligi kuu ya England

Southampton 1-0 Manchester United

Haki miliki ya picha epa
Image caption Southampton 1-0 Manchester United

12:27

LOOOOOOO

Sadio Mané (Southampton) anafyatua mkwaju wa haja hapa

11:46 free kick

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashabiki nao wamejitokeza kwa wingi

Memphis Depay (Manchester United)

2:41

Haki miliki ya picha epa

Victor Wanyama (Southampton) anacheza visivyo.

1:31free kick

Michael Carrick (Manchester United)

Ref: Mark Clattenburg

Haki miliki ya picha PA
Image caption Van Gaal

Timu ya Southampton

22 Stekelenburg 03 Yoshida 06 Fonte 17 van Dijk 33 Targett 12 Wanyama 14 Romeu 10 Mané 16 Ward-Prowse 11 Tadic 19 Pellè

Image caption Southampton katika mechi ya awali

Wachezaji wa akiba

01 Davis 02 Soares 07 Long 08 Davis 09 Rodriguez 15 Martina 20 Juanmi

Timu ya Manchester United

Image caption de Gea amerejea kwa kishindo

01 de Gea 36 Darmian 12 Smalling 17 Blind 05 Rojo 16 Carrick 28 Schneiderlin 08 Mata 10 Rooney 07 Depay 09 Martial

Wachezaji wa akiba

18 Young 20 Romero 21 Herrera 25 A Valencia 27 Fellaini 31 Schweinsteiger 33 McNair