Louis Van Gaal amwaga tambo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kocha wa Manchester United

Meneja wa Klabu ya Manchester United Louis van Gaal ambaye baada ya Ushindi wa jana mabao 3-2 dhidi ya Southampton sasa amesema kikosi chake kina uwezo wa kuchukua ubingwa wa Ligi ya England katika msimu huu wa ligi.

Ushindi huo umemfanya Mholanzi huyo kuendelea kukiamini kikosi chake huku kinda wa timu hiyo Anthony Martial aking'ara kwa kuweka kimiani magoli 2.

Ushindi huo umeipeleka klabu ya Man U mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nyuma ya vinara Manchester City waliopoteza katika mchezo katika mchzo dhidi ya West Ham 2-1 siku ya jumamosi. Matokeo mengine Tottenham iliichapanga Crystal Palace 1 - 0. Liverpool ikitoka sare ya 1 kwa 1 Norwich City.