Jack Warner akanusha mashtaka yake

Haki miliki ya picha Warner TV
Image caption Jack Warner akanusha mashataka dhidi yake

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Trinidad na Tobago ametoa kibali juu ya kesi iliyofunguliwa na Marekani dhidi ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Jack Warner.

Anatuhumiwa kuhusika kupokea mamilioni ya dola za kimarekani kama rushwa alipokuwa madarakani.

Warner pamoja na maofisa wengine kumi na watatu wa sasa na wa zamani wa FIFA walipewa mashitaka na mamlaka ya Marekani tokea mwezi Mei mwaka huu.

Warner amekanusha mashitaka yanayomkabili. Juma lililopita, serikali ya Switzerland ilithibitisha kuachiliwa kwa Kiongozi mwingine wa FIFA Eugenio Figueredo kutoka Uruguay. Figueredo alikamatwa mwezi Mei alipokwenda nchini humo kwa shughuli za kikazi za FIFA.