Rodgers wa Liverpool aambiwa ana mtihani

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers

Meneja wa klabu ya soka ya Liverpool Brendan Rodgers atakua na siku kumi ngumu za kibarua chake katika timu hiyo, hayo yamesemwa na mlinzi wa zamani wa timu hiyo Mark Lawrenson.

Liverpool ilipata ushindi wa matuta wa 3-2 dhidi ya klabu ya daraja la pili ya Carslisle baada ya kuishia na sare ya 1-1.

Liverpool itakutana na Aston Villa na kisha Everton katika michezo inayofuata ya ligi kuu England.

Lawrenson amesema kuwa Rodgers ''yupo katika hatari kubwa'' na timu hiyo imekosa hamasa.

Akizungumza na BBC, ameongeza kuwa ''Sipendelei kuona waalimu wa vilabu wakifukuzwa mara kwa mara kwa sababu najua ni miongoni mwa kazi ngumu ila sio kwa michezo sita zaidi ya ushindi wa matuta ulioipata dhidi ya klabu ya daraja la pili''