Raga: New Zealand yaibwaga Namibia

Haki miliki ya picha ALL SPORT Getty
Image caption timu ya rugby ya New Zealand

Mabingwa watetezi New Zealand wameondoka na ushindi mnene wa 58-14 dhidi ya wawakilishi pekee wa Afrika waliokuwa wamesalia katika michuano hiyo ya dunia Namibia katika uwanja wa Olimpiki London.

Namibia ambayo ipo chini katika viwango vya dunia,hawakuweza kuonyesha upinzani mkubwa kwa New Zealand walioonekana kuwa bora zaidi yao.

New Zealand walifunga mara tano kabla ya mapumziko kabla ya kufunga tena mara nne katika kipindi cha pili.

Namibia waliinuka zaidi kipindi cha pili lakini hali bado ikaendelea kuwa ngumu mbele ya wababe wa dunia New Zealand.