Uefa:ligi kuendelea leo

Image caption Ligi ya Uefa kuendelea jumanne

Michezo ya pili ya michuano ya klabu bingwa itaendelea tena kushika kasi baadaye leo usiku kwa michezo nane .

Katika kundi E Barcelona itakua katika dimba lao la Camp Nou, kuwaalika Bayern Leverkusen kutoka Ujerumani mchezo huku Bate wakiwaalika As Roma mchezo utaopigwa katika uwanja wa Borisov-Arena.

Katika kundi F Arsenal ya England itakipiga na Olympiakos ya Ugiriki, wakati miamba wa Ujerumani Bayern Munich wao wakishuka dimbani kuwakabili Dinamo Zagreb ya Croatia.

Ratiba kamili ya mechi za leo usiku

Barcelona vs Bayer Levkn

Arsenal vs Olympiakos

Bayern Mun vs Dinamo Zagreb

FC Porto vs Chelsea

BATE Bor vs Roma

Maccabi Tel Aviv vs Dynamo Kiev

Lyon vs Valencia

Zenit St P vs KAA Gent