Kriketi: Kocha wa West Indies atimuliwa

Image caption Kocha wa West Indies, Phil Simmons

Timu ya Kriketi ya West Indies imemtimua kocha wake mkuu Phil Simmons baada ya kushutumiwa kuchagua timu vibaya.

Simmon mwenye umri wa miaka 52 aliyechaguliwa kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho mwezi machi mwaka huu amelaumiwa kwa kuwaengua Dwayne Bravo na Kieron Pollard, katika safari ya kuelekea Sri Lanka.

Eldine Baptiste, amechaguliwa kuwa mkufunzi wa kikosi kitachokwenda kushiriki michuano itakayoanza Octoba 14 nchini Sri Lanka.

Mwenyekiti wa bodi ya mchezo wa kriketi ya West Indies, amethibitisha kuwa kocha huyo ameondolewa kwenye timu na hatosafiri na timu.