Ligi kuu Tanzania kuendelea leo

Image caption Kikosi cha Yanga

Ligi Kuu ya Tanzania bara itaendelea tena leo kwa timu 14 kujitupa katika viwanja saba nchini.

Simba SC watakua wenyeji wa Stand United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Azam FC watawakaribisha Coastal Union kwenye uwanja wa Azam Complex – Chamazi jijini Dar es salaam.

Mjini Morogoro vinara wa ligi hiyo Young Africans watakua ugenini kuwakabili wenyeji Mtibwa Sugar Wana Lizombe Majimaji FC watakua wenyeji wa Ndanda FC kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Wakata Miwa wa Kagera Sugar watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, African Sports wakiwakaribisha wa Mgambo Shooting uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Tanzania Prisons wakiwa wenyeji wa Mwadui FC katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea siku ya Alhamisi kwa mchezo mmoja ambapo Toto Africans watakuwa wenyeji wa Mbeya City katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.