Uefa:Klabu bingwa ulaya kuendelea leo

Image caption Kikosi cha Manchester United

Ligi ya mabingwa ulaya itaendelea kutimua vumbi leo kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja tofauti.

Katika kundi A Malmo FF, watakua wenyeji wa Real Madrid ,mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Swedbank Stadion, Huku Shakhtar Donetsk wakipepetana na Paris St Germaini.

CSKA Moscow wao watawalika Psv wakati Manchester United, wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Old Trafford, kucheza na VfL Wolfsburg, hii ni michezo ya kundi B.

FC Astana watapima na ubavu na Galatasaray ya Uturuki, mchezo mwingine wa kundi hilo C utakua kati ya Atletico Madrid na Benfica.

Borussia Mönchengladbach wao watakua nyumbani Ujerumani kuwakaribisha Man City toka England, huku Juventus ya Uitaliano ikikipiga na Wahispania wa Sevilla.