Yanga na Simba zapata ushindi

Image caption Msimamo wa Ligi kuu Tanzania

Vigogo wa soka nchi Tanzania Yanga, Simba pamoja na Azam FC wamendeleza wimbi la ushindi katika michezo ya ligu kuu.

Yanga waliokua ugenini mjini Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar walipata ushindi wa mabao 2-0 kwa mabao ya Malimi Busungu na Donald Ngoma na kuifanya yanga iendelee kuongoza ligi kwa alama 15.

Azam nao wakicheza katika dimba lao la Azam Complex waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhid ya Coastal Union ya Tanga, mabao ya Azam yakifugwa na Shomari Kapombe na Kipre Tche Tche.

Wekundu wa Msimbazi Simba wakawachapa Stand United kwa bao 1-0 bao hilo pekee likiwekwa kimiani na Joseph Kimwaga.

Matokeo mengine ya michezo ya ligi hiyo

African Sports 0-1 Mgambo

Kagera Sugar 0-0 JKT Ruvu

Majimaji FC 1-1 Ndanda FC

Prisons 0-0 Mwadui FC 0