Man United, City zang'aa Ulaya

Image caption Kikosi cha Manchester United

Timu za Jiji la Manchester, Man United na Man City zimefanyikiwa kupata ushindi wake wa kwanza katika michuano ya klabu bingwa ulaya msimu huu.

Man United wakiwa katika dimba lao la Old Trafford walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Vfl Wolfsburg, Daniel Caligiuri alianza kuwaandikia Wolfsburg bao la mapema kabla ya Juan Mata kusawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penati na baadae Chriss Smalling kufunga bao la ushindi.

Man City wakicheza ugenini walipata ushindi kwa kuichabanga timu ya Borrusia Monchenglabach kwa mabao 2-1 mabao ya City yakifungwa na Nicolas Otamend na Sergio Aguero huku lile la Borrusia Monchenglabach likifungwa na Lars Stindl.

Katika mchezo mwingine Real Madrid waliibuka na ushindi dhidi ya Malmo kwa mabao 2-0 mabao yote yakiwekwa kimiani na Cristiano Ronaldo na kufanikiwa kufikisha mabao 500 akiwa mchezaji wa soka la kulipwa.

Matokeo mengine ya klabu bingwa barani ulaya

Shakhtar Donetsk 0 -3vParis St Germaine

CSKA 3-2 PSV

FC Astana 2 -2 Galatasaray

Atletico Madrid 1 -2 Benfica 2

Juventus 2-0 Sevilla