Venus Williams amshinda Konta

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Venus Williams amdhibiti Johanna Konta

Muingereza Johanna Konta amefungwa na nyota namba moja wa zamani wa mchezo wa tenesi Mmarekani Venus Williams.

Konta alipoteza mchezo huo wa nusu fainali ya michuano ya wazi ya Wuhan kwa seti 6-4 3-6 7-5.

Muingereza huyo aliyeshinda michezo 21 katika yake 22 iliyopita alimshinda mchezaji namba mbili kwa ubora wa mchezo huo kwa upande wa wanawake Simona Halep siku ya jumatano.

Konta alianza mwaka akiwa katika nafasi ya 150 lakini kwa sasa yuko katika nafasi ya 66 kwa ubora wa viwango vya mchezo huo.