TP Mazembe kukutana na Alger fainali

Image caption Timu ya TP Mazembe

Klabu ya TP Mazembe ya Congo DRC, Itakutana na klabu ya Algeria USM Alger katika hatua ya fainali ya klabu bingwa barani Afrika.

Mazembe ilijihakikishia nafasi yake siku ya jumapili yaani jana baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya El Merrekh ya Sudan mjini Lubumbashi. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta alifunga mara mbili katika ushindi huo huku Muivarycoast Roger Assale akifunga goli la tatu.