Jose Mourinho ashitakiwa kwa utovu wa nidhamu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Morinho ashitakiwa FA

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho ameshitakiwa na chama cha soka nchini Uingereza FA kutokana na utovu wa nidhamu baada ya matamshi yake juu ya maafisa wa soka wa FA kuhusika kwenye kichapo cha goli 3-1 dhidi ya Southampton siku ya jumamosi.

FA imedai kwamba maoni hayo yalikuwa yakijaribu kuashiria kwamba kulikua na upendeleo kwa upande fulani. Mourinho alimlalamikia mwamuzi Robert Madley kwa kuwakatalia Chelsea penalti siku ya jumamosi na kusema kuwa maofisa wa mchezo walikuwa hawataki timu yake ishinde mchezo huo. Mreno huyo mwenye miaka 52 amepewa hadi Oktoba 8 kujibu tuhuma hizo. Kwa kufungwa na Southampton ina maana kuwa Chelsea imepoteza michezo minne kati ya minane ya ufunguzi wa ligi msimu huu huku wakiwa alama 10 nyuma ya vinara Manchester City na alama 4 juu ya mstari wa kushuka daraja