Jurgen Klopp kutua Liverpool Ijumaa?

Image caption Jurgen Klopp

Klabu ya soka ya Liverpool imetangaza kuwa ina matumaini ya kumteua Jurgen Klopp kuwa meneja mpya wa klabu hiyo ifikapo siku ya ijumaa wiki hii.

Mazungumzo kati ya klabu ya Liverpool na wawakilishi wa Klopp ambaye ni kocha wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund yanaendelea kuangalia uwezekano wa kuchukua nafasi ya meneja aliyetimuliwa Brendan Rodgers. Klopp mwenye miaka 48 raia wa Ujerumani ameweka wazi mipango ya kujiunga na klabu yoyote kwa sasa. Wamiliki wa klabu hiyo wamepanga kupata mwalimu mpya kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tottenham tar 17 mwezi Oktoba.

Katika taarifa iliyotolewa na chama cha mameneja wa ligi hiyo kwa niaba ya Rodgers imeelezea kusikitishwa kwake na tukio la kutimuliwa kwa kocha huyo. ''imekuwa heshima na upendeleo wa kipekee kwangu kuiongoza klabu ya Liverpool hususan katika michezo migumu''alisema Rodgers aliyetimuliwa baada ya suluhu ya bao 1-1 dhidi ya Everton siku ya jumapili.