Liverpool kupata kocha mpya?

Image caption Jurgen Klopp

Klabu ya Liverpool inakaribia kumteua meneja wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund Jurgen Klopp.

Majogoo hao wa jiji la Liverpool wanatarajiwa kukamilisha makubaliano yao siku ya Alhamisi na Klopp raia wa Ujerumani kuchukua rasmi mikoba ya Brendan Rodgers mwishoni mwa juma hili, kwa mkataba wa miaka mitatu.

Rodgers alitimuliwa siku ya Jumapili kufuatia suluhu ya 1-1 dhidi ya Everton katika mchezo wa ligi kuu ya England.

Klopp ameomba kuambatana na wasaidizi wake wawili wa zamani katika benchi la ufundi ambao ni Zeljko Buvac na Peter Krawietz.

Buvac raia wa Bosnia mwenye miaka 54 na mjerumani Krawietz mwenye miaka 43, walitoa ushirikiano mzuri na kupata mafanikio makubwa wakifanya kazi pamoja klabuni Borussia Dortmund.