Sudan Kusini yatoka sare na Mauritania

Sudan Kusini
Image caption Mechi ilisimamishwa timu zote mbili zikiwa sare 1-1

Timu ya soka ya Sudan Kusini, almaarufu Bright Star, imepata alama yake ya kwanza kwenye mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Hii ni baada ya timu hiyo kutoka sare ya 1-1 na Mauritania baada ya mechi iliyosimamishwa jana kuendelea leo.

Mechi hiyo, ambayo ni ya kwanza kabisa ya Sudan Kusini katika kampeni ya kufuzu kwa Kombe la Dunia ilisitishwa siku ya kwanza kutokana na mvua kubwa baada ya kuchezwa dakika 10 pekee.

Mechi hiyo ya mkondo wa kwanza, iliyokuwa ikichezewa mjini Juba, ilisimamishwa mambo yakiwa 1-1 kati yao na Mauritania na leo mambo yalisalia vivyo hivyo.

Sudan Kusini ilionyesha mchezo mzuri mbele ya mashabiki wa nyumbani na kudumisha bao waliliojipa hapo jana kupitia Dominic Abui Pretino katika dakika ya tano baada ya Boubacar Bagili kuiweka Mauritania kifua mbele kunako dakika ya tatu.

Bao hilo ni lao la kwanza kabisa katika kinyang'anyiro cha Kombe la Dunia.

Mataifa hayo mawili yanatarajiwa kukutana tena kwa mechi ya marudiano mjini Nouakchott Jumanne Oktoba 13.

South Sudan ilianza kucheza soka ya kimataifa 2012, mwaka mmoja baada ya kupata uhuru kutoka kwa Sudan.

Mwezi uliopita, waliandikisha ushindi wao wa kwanza kabisa mechi ya ushindani walipolaza Equatorial Guinea 1-0 mechi ya kufuzu kwa Kombe la Taifa Bingwa Afrika 2017.Full time at Juba Stadium, with the match between South Sudan and Mauritania ending in a 1-1 draw.