Pacquiao kupigana mara ya mwisho

Haki miliki ya picha AP
Image caption Manny Pacquiao

Bondia raia wa Ufilipino Manny Pacquiao amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa akastaafu katika ulingo wa ndondi baada ya pigano moja mwaka ujao.

Pacquiao,ambaye alipoteza kwa Floyd Mayweather katika pigano la mwisho ,anataka kuwania kiti kimoja katika bunge la seneti mwaka 2016.

Raia wa Uingereza Amir Khan ni mmoja ya wapinzani wa Pacquiao mwenye umri wa miaka 36,huku Terence Crwaford kutoka Marekani akiwa mpinzani mwengine.

''Nadhani niko tayari.Nimepigana ndondi kwa zaidi ya miaka 20'',bingwa huyo wa dunia katika uzani 6 tofauti aliambia ANC.

''Unapokuwa seneta,lengo lako linakuwa kazi yako na familia,Nitahitajika kuwacha mambo mengine ambayo yanahitaji kupewa kipaumbele''.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mayweather na Manny Pacquiao baada ya pigano

Pacquiao amesema kuwa ''hawezi kusema'' iwapo pigano lake la mwisho litakuwa dhidi ya Mayweather,baada ya raia huyo wa Marekani kuahidi kustaafu baada ya ushindi wake dhidi ya Andre Berto.

Raia huyo wa Ufilipino ,ambaye alifanyiwa upasuaji katika bega lake baada ya pigano lake na Mayweather,anajivunia rekodi ya mapigano 57,kushindwa mara 6 na sare ya mapigano 2.