Sergio Aguero na Silva wapata majeraha

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sergio Aguero

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Sergio Aguero anatarajiwa kukaa nje kwa mwezi mmoja baada ya kupata jeraha nyuma ya goti lake wakati alipokuwa akiichezea Argentina.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27,ambaye alifunga mabao matano pekee katika ushindi wa klabu ya City dhidi ya Newcastle wikiendi iliopita ,alicheza kwa dakika 22 pekee wakati timu Argentina iliposhindwa na Ecuador.

Image caption David Silva

''Nadhani nitakuwa nje kwa kipindi cha mwezi mmoja'' ,Aguero aliiambia TYC Sport katika mji mkuu wa Bueno Aires.

Matatizo ya City vilevile yaliongezeka baada ya David Silva kutoka katika mechi ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Luxembourg baada ya kuteguka kifundo cha mguu.