Hamilton ashinda tena huko Russia

Image caption Hamilton ashinda tena huko Russia

Dereva wa Mercedes Lewis Hamilton aliibuka mshindi wa mkumbo wa Russia wa mbio za magari ya langalanga katika shindano lililokumbwa na ajali nyingi.

Kufuatia ushindi huo mkubwa raia huyo wa Uingereza amekaribia sasa kutawazwa mshindi wa mwaka huu wa mbio za magari ya langalanga ubingwa wake wa tatu wa dunia

Hamilton alikuwa katika nafasi ya pili kuelekea dakika za mwisho mwisho za mashindano hayo kabla ya dereva mwenza wa Mercedes Nico Rosberg kukabiliwa na matatizo ya injini.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Hamilton alikuwa katika nafasi ya pili kuelekea dakika za mwisho mwisho za mashindano hayo kabla ya dereva mwenza wa Mercedes Nico Rosberg kukabiliwa na matatizo ya injini.

Mjerumani huyo alilazimika kuyaaga mashindano aliposhindwa kupata kasi .

Dereva wa Ferrari Sebastian Vettel alimpiku Rosberg kutoka katika nafasi ya pili katika jedwali la msimamo wa dereva bora msimu huu.

Dereva wa Force India, Sergio Perez alimaliza katika nafasi ya tatu baada ya dereva shupavu wa Ferrari, Kimi Raikkonen, kuhusika katika ajali mbaya na gari la Williams lililokuwa likiendeshwa na Valtteri Bottas katika mzunguko wa mwisho.

ALAMA 9

Hamilton ameshinda sasa mashindano 9 msimu huu na hivyo anahitaji alama 9 pekee kutawazwa bingwa mara tatu duniani.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Hamilton ameshinda sasa mashindano 9 msimu huu

Mashindano yajayo yatakuwa Marekani.

Licha ya kumaliza katika nafasi ya 5 Raikkonen alipata pigo alipoadhibiwa kwa kusababisha ajali na hivyo alimaliza katika nafasi ya 8.

Ushindi huu hata hivyo umeikabidhi Mercedes taji la mwaka huu la watengenezaji magari.